Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Makundi ya wadudu waharibifu

Wadudu waharibifu wanaweza kugawanywa katika makundi mawili (2) ambayo ni;
  • Wanaoshambulia chini ya ardhi (mbegu na mizizi), na
  • Wanaoshambulia juu ya ardhi (wanaotafuna majani, wanaotoboa mashina, wanaonyonya utomvu au majimaji ya mmea na wanaokula hariri (nyuzi za mahindi))
Pia, wadudu waharibifu wanaweza kugawanywa zaidi na kupatikana makundi manne (4) ambayo ni;
  • Wadudu wanaoshambulia mbegu, mizizi na miche
  • Wadudu wanaoshambulia majani na sehemu ya juu ya maua ya mhindi (tassel)
  • Wadudu wanaoshambulia mashina, mhindi uliozalishwa (ear) na sehemu ya juu ya maua ya mhindi (tassel)
  • Wadudu wanaoshambulia mhindi uliozalishwa (ear) na punje za mahindi (grain)
Wadudu wanaweza kushambulia na kuharibu mbegu za mahindi kabla hazijaota, na hivyo kusababisha baadhi ya mahindi yaliyopandwa kushindwa kuota. Kukabiliana na changamoto hii tumia mbegu ambazo zimewekewa dawa ambazo umezinunua au umeweka dawa mwenyewe. Aina ya dawa ambayo imewekwa kwenye mbegu inategemena na wadudu ambao umelenga kukabiliana nao.

Matumizi ya mbegu zenye dawa huweza kusaidia sana sehemu zenye historia ya wadudu au minyoo kama sod, alfalfa, reduced tillage (kulima kidogo), na/ au udongo wa hilo shamba hufanya mbegu zichelewe kuota.

Kuwa na tahadhari zaidi ikitokea wakati unalima hilo shamba au kuliandaa uonapo dalili za wadudu wengi wabaya kama seed corn maggot flies, seed corn beetles, and/or wireworms. Hii itafanya uamue kutumia mbegu zenye dawa.

Wadudu wanaopogoa au kukata mizizi na wale wanaotafuna mabua au mashina ni pamoja na corn rootworm larvae, wireworm larvae, and white grubs. Baadhi ya madawa yaliyopakwa kwenye mbegu hayakingi mbegu dhidi ya wadudu baada ya mbegu kupasuka na kuanza kuota.

Wadudu wanaoshambulia mahindi juu ya ardhi ni pamoja na; thrips, flea beetles, chinch bugs, stalk borers, cutworms, and garden webworms.

Juu ya wadudu shambani pia soma; Wadudu wa faida shambani, na Makundi ya wadudu waharibifu shambani.