Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Wadudu wa faida shambani
Kudhibiti wadudu shambani ni moja ya sababu kuu ya kutumia kemikali shambani. Hata hivyo wapo wadudu shambani ambao sio waharibifu badala yake husaidia sana mazao kustawi. Hawa ni wadudu wenye faida kwa mkulima na mazao kwasababu huangamiza wadudu waharibifu wa mazao. Baadhi yao ni;
- Pirate bugs or flower bugs – hudhuru au hula (prey) thrips, mites, mayai ya wadudu, aphids
- Lacewings – hudhuru au hula (prey) aphids, thrips, mayai ya wadudu, very young larvae, mites
- Black hunting wasps – huwinda armyworms
- Assassin bugs - hudhuru au hula (prey) beetles, froghoppers na minyoo
- Lady beetles – hula aphids, mites, insect eggs, small insect larvae
- Tiny wasps - parasitize armyworm eggs
- Minute wasps – parasitize stem borer moth eggs
Kiwango cha wadudu waharibifu kwenye shamba la mahindi hubadilika kuendana na vitu vingi kama; msimu na mabadiliko ya hali ya hewa, maandalizi na shamba na jinsi shamba lilivyolimwa, kiasi na ubora wa chakula cha wadudu, mashindano kati ya wadudu aina moja na kati ya wadudu wa aina tofauti, magonjwa ya milipuko (epidemics) ya virusi, bakteria na fangasi, kiwango cha wadudu/ wanyama/ ndege wanaowinda au kula wadudu na kiwango cha wadudu (predator and parasite population).
Ikumbukwe pia kuwa wadudu huwa waharibifu shambani pale inapotokea idadi yao au / na uharibifu wao umezidi kiwango kinachokubalika (economic threshold), na hivyo kuanza kuwa tishio kwa mkulima.
Juu ya wadudu shambani pia soma;
Wadudu wa faida shambani, na
Makundi ya wadudu waharibifu shambani.