Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Maandalizi ya Shamba

Katika sehemu hii tutazungumzia; kazi katika kuandaa shamba, matumizi ya moto, njia za kulima na zana za kulimia, mahitaji ya mahindi (udongo unaofaa na hali ya hewa inayofaa) na vitu vinavyosababisha rutuba kupotea kutoka kwenye shamba.

Kuandaa Shamba

Kimsingi, njia yoyote inaweza kutumika ilimradi nyasi na magugu viweze kutolewa shambani na udongo uweze kutifuliwa tifuliwa.

Wakati wa Kuandaa Shamba

Kuandaa shamba kwa kipindi sahihi ni muhimu sana. Maandalizi ya shamba yaanze mavuno yakikamilika au angalau wiki tatu (3) kabla hujapanda mahindi. Hii itawezesha kuoza kwa nyasi, mimea na majani shambani. Lima shamba angalau mara mbili kupata udongo ambao umevurugwa kiasi. Usilime sana udongo ukalainika sana maana mvua zikinyesha itakuwa rahisi udongo kusombwa (mmonyoko wa udongo) na maji ya mvua na hivyo kusababisha rutuba kupotea na shamba kuharibika.