Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Maandalizi ya Shamba

Katika sehemu hii tutazungumzia; kazi katika kuandaa shamba, matumizi ya moto, njia za kulima na zana za kulimia, mahitaji ya mahindi (udongo unaofaa na hali ya hewa inayofaa) na vitu vinavyosababisha rutuba kupotea kutoka kwenye shamba.

Matumizi ya Moto

Kuna hoja kadhaa kuhusu matumizi ya moto katika kuandaa shamba. Wanaounga mkono matumizi ya moto katika kuandaa mashamba husema kuwa;

  • Bila ya kuchoma moto miti, matawi ya miti, magugu, nyasi na majani mengine kwenye shamba linaloandaliwa kwa hudaiwa kuwa kazi ya kuandaa shamba huchukua muda mrefu ukilinganisha na kuchoma moto na maandalizi huwa na gharama zaidi. Sababu ni kuwa huchukua muda mrefu kuoza kwa majani, miti, nyasi na mabaki mengine ukilinganisha na kuyachoma moto ambapo inakuwa kazi ya siku chache tu.
  • Kutokuchoma moto huzalisha na kutunza wadudu na magonjwa ya mazao kutoka kwenye malundo ya matawi ya miti, nyasi, magugu na mimea ingine na hivyo kuhatarisha usalama wa mazao. Hii hutokea zaidi pale mabaki haya ya mimea yasipooza vizuri
  • Kuna tafiti zinaonyesha kuwa kuna madini yanapatikana kwa kuchoma moto majani, nyasi, magugu na mimea mingine shambani na kwamba madini hayo hupunguza kiwango cha tindikali (acid) kwenye udongo na kuufanya uwe wa alkali na wenye rutuba

Moto ni muhimu?

Kundi la wanaopinga kuchoma moto nyasi, miti na matawi yake, magugu na mimea mingine kwenye shamba linaloandaliwa kwa kilimo hudai kuwa;
  • Ukichoma moto majani, nyasi na mimea mingine shambani utaharibu virutubisho muhimu katika udongo ambavyo kuvirudishia ni ngumu sana
  • Matumizi ya moto huharibu afya na mazingira
  • Moto usipodhibitiwa vizuri huweza kusambaa na kuteketeza sehemu ambayo haikukusidiwa na hivyo kusababisha hasara na matatizo mengine
  • Hata hivyo hukubali kuwa moto unaweza kutumika kuunguza au kuondoa magugu mabaya shambani pamoja na kuzuia magonjwa na wadudu haribifu
Moto uliowashwa kuandaa shamba Moto ukiunguza sehemu ambayo haikulengwa