Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Maandalizi ya Shamba

Katika sehemu hii tutazungumzia; kazi katika kuandaa shamba, matumizi ya moto, njia za kulima na zana za kulimia, mahitaji ya mahindi (udongo unaofaa na hali ya hewa inayofaa) na vitu vinavyosababisha rutuba kupotea kutoka kwenye shamba.

Mahitaji ya Mahindi

Kimsingi, udongo wa shamba la kupanda mahindi unatakiwa uwe na sifa zifuatazo;

  • Wenye rutuba mpaka chini zaidi (sio rutuba ya juu juu tu kwenye udongo). Mara nyingi udongo mweusi huwa na rutuba inayokuwa imesababishwa na kuoza kwa nyasi na mimea mingine.
  • Uwe wenye jotojoto na wenye unyevunyevu
  • Uwe unapitisha hewa kwa urahisi
  • Uweze kuruhusu kuota kwa mbegu haraka na mizizi kukua vizuri kuweza kufyonza virutubisho vilivyo kwenye udongo. Udongo ulioandaliwa vizuri unapunguza nyasi katika shamba na hivyo kupunguza kazi ya palizi
  • Uwe na rutuba, wa kichanga kingi kuliko clay na silt na usioweza kutuamisha maji. Usiofaa ni upi? Focus on local soils when explaining on suitable and unsuitable soils
  • Wenye muundo usio wakushikamana sana ambao utaruhusu maji na hewa kupita kwa kasi na hivyo kutotuamisha maji
  • Wenye udongo mfinyanzi chini ya 7%, silt chini ya 50% na kichanga kati ya 43% na 50% au udongo wenye mchanganyiko wa udongo mfinyanzi, kichanga na silt na ambao una rutuba
  • Udongo wenye mchanganyiko wa udongo mfinyanzi, silt na kichanga ukiufinyanga mkononi unafinyangika na ukiubonyeza kidogo unatawanyika
  • Kiwango cha asidi na alkali katika udondo kati ya pH 5.0 – 7.0
  • Ishara za rutuba kwenye udongo kama vile uoto wa nyasi na mimea kama guinea grass, elephant grass
Kushoto udongo usio na rutuba, kulia wenye rutuba Kushoto udongo usio na rutuba, kulia wenye rutuba

Shamba la mahindi halitakiwi kuwa na udongo wenye sifa zifuatazo;

Shamba la mahindi halitakiwi kuwa na udongo wenye sifa zifuatazo;
  • Unaotuamisha maji maana mahindi hayataki udongo unaotuamisha maji
  • Una mchanga mwingi na hivyo kupitisha na kupoteza maji na virutubisho haraka sana
  • Ni mfinyazi na ambao una alkali nyingi au tindikali (acid) nyingi
  • Hauna rutuba
Udongo wenye kutuamisha maji Mahindi yamestawi kwenye udongo wenye mchanga mwingi. Teknolojia ya surface water retention (SWRT) imetumika.