Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Maandalizi ya Shamba

Katika sehemu hii tutazungumzia; kazi katika kuandaa shamba, matumizi ya moto, njia za kulima na zana za kulimia, mahitaji ya mahindi (udongo unaofaa na hali ya hewa inayofaa) na vitu vinavyosababisha rutuba kupotea kutoka kwenye shamba.

Baadhi ya Kazi katika Kuandaa Shamba

Kutegemeana na shamba, kazi ya kuandaa shamba la mahindi kunaweza kuhusisha kazi mbalimbali, baadhi ni;
  • Kukata miti na vichaka
  • Kung’oa visiki
  • Kuondoa mawe kama yamo
  • Kuondoa vichuguu vya mchwa
  • Kufyeka nyasi kama nyasi ni ndefu na ziache shambani humohumo baada ya kufyeka
  • Tumia vifaa vinavyofaa kufukia mabaki ya mimea na nyasi humohumo shambani. Hii itasaidia udongo kuhifadhi unyevunyevu, kuongeza uwezo wake wa kuhifadhi na kupenyeza maji na kuongeza rutuba ya udongo
  • Kama shamba lilikuwa na nyasi au mimea kama Amaranthus ssp ambayo hutoa mbegu nyingi, inabidi kuandaa shamba mapema. Hii itafanya mbegu za hizo nyasi na mimea kuota haraka udongo utakapopata unyevunyevu. Halafu shamba itabidi lilimwe kiasi au kunyunyiziwa kemikali kama glyphosates kabla mahindi hayajapandwa
Ondoa vichaka Kata nyasi zibaki fupi
Ondoa vichuguu Ng'oa visiki shambani