Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Mbegu na Kupanda

Sehemu hii tutazungumzia; madaraja ya mbegu na faida za matumizi ya mbegu bora, kuchagua mbegu bora, kuangalia uotaji wa mbegu, muda wa kupanda, kina cha mashimo, na jinsi ya kupanda.

Madaraja ya Mbegu

Kwa mujibu wa kipeperushi cha Wizara ya Kilimo Tanzania, Mbegu ni sehemu ya mmea ambayo hutumika kwa ajili ya kupanda ili kuzalisha mazao na inabidi iwe na uwezo wa kuota vizuri, iliyo safi, iliyokauka vizuri na isiyo na magonjwa.
Hapa Tanzania mbegu ziko katika madaraja manne (4) ambayo ni;

  • Mbegu mama – huzalishwa na watafiti
  • Mbegu ya msingi – huzalishwa na Wakala wa Mbegu wa Taifa (ASA), na Makampuni yaliyoidhinishwa kuzalisha Mbegu zenye Haki Miliki
  • Mbegu ya kuthibitishwa ubora daraja la I na la II – huzalishwa na ASA na makampuni ya Mbegu
  • Daraja la kuazimiwa ubora – huzalishwa na wakulima wadogo waliofundishwa na kusajiliwa

Faida za Mbegu bora

Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo Tanzania, matumizi ya Mbegu bora zina faida zifuatazo katika Kilimo;

  • Huongeza kiwango cha mavuno
  • Hustahimili magonjwa, na wadudu waharibifu
  • Hupunguza gharama za kurudishia Mbegu shambani kutokana na uotaji mzuri
  • Hutoa mavuno mazuri yanayokubalika sokoni na kumuongezea mkulima kipato

Angalia video hapa chini juu ya mbegu na mbolea ya kupandia;