Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Mbegu na Kupanda

Sehemu hii tutazungumzia; madaraja ya mbegu na faida za matumizi ya mbegu bora, kuchagua mbegu bora, kuangalia uotaji wa mbegu, muda wa kupanda, kina cha mashimo, na jinsi ya kupanda.

Upandaji

Kupanda mahindi, unaweza kutumia mashine au mkono. Na unaweza kupanda kwenye matuta au kwenye tambarare. Zingatia yafuatayo;

  • Panda mvua zinapoanza. Kupanda mapema ni vizuri maana Nitrogen iliyokusanyika kwenye udongo kipindi cha kiangazi inatoka na kusaidia mahindi
  • Epuka kuchelewa kupanda maana itaongeza uwezekano wa mazao yako kushambuliwa na wadudu haribifu na magonjwa
  • Panda kwa mstari ili kupanda mbegu nyingi zaidi na pia kurahisisha kazi za palizi, kunyunyizia madawa na mbolea na kuvuna
  • Kwenye shimo weka mbegu 1 mpaka 3. Umbali kati ya mstari na mstari iwe sm 75 – 85, na sm 25 – 40 iwe kwa umbali kati ya shimo na shimo
  • Umbali mkubwa kati ya shimo na shimo husababisha nyasi na magugu kuota zaidi na mmomonyoko wa udongo kutokea
  • Umbali kati ya shimo na shimo hutegemea rutuba ya udongo, aina ya mmea, ukuaji wake, kiasi cha mvua, na lengo la kulima hilo zao
  • Baada ya kuweka mbegu kwenye shimo, lifukie na udongo
  • Shimo la kupanda mahindi lnaweza kuchimbwa kwa kijiti au jembe

Angalia video hizi hapa chini zenye maelekezo ya jinsi ya kupanda kwa kamba;