Mbegu na Kupanda
Sehemu hii tutazungumzia;
madaraja ya mbegu na faida za matumizi ya mbegu bora,
kuchagua mbegu bora,
kuangalia uotaji wa mbegu,
muda wa kupanda,
kina cha mashimo,
na jinsi ya kupanda.
Kina cha Mashimo
Ni muhimu kuwa makini unapochimba mashimo kwa ajili ya kupanda mahindi. Kina cha mashimo kizingatie yafuatayo;
- Mashimo yawe na kina cha sm 3 – 8
- Kina kizingatie unyevunyevu wa udongo, hali ya hewa, na joto
- Kina kifupi cha sm 2 – 4 kinafaa kwa udongo wenye unyevu, wakati kina kirefu kati ya sm 5 – 8 kinafaa kwa udongo mkavu. Mashimo yenye kina kirefu yanashauriwa kwa udongo mkavu ili mbegu ziote tu pale ambapo mvua za kutosha zimenyesha
- Hakikisha shamba lote lina mashimo yanayofanana kina ili ukuaji uwe sawa kwa shamba lote
|
Mkulima akiandaa mashimo tayari kupanda mahindi |