Mbegu na Kupanda
Sehemu hii tutazungumzia;
madaraja ya mbegu na faida za matumizi ya mbegu bora,
kuchagua mbegu bora,
kuangalia uotaji wa mbegu,
muda wa kupanda,
kina cha mashimo,
na jinsi ya kupanda.
Kuchagua mbegu bora
Kimsingi mavuno mengi na bora huanza na mbegu bora. Unashauriwa kutumia mbegu zilizoboreshwa kwa kilimo chako. Kama huna mbegu zako mwenyewe hakikisha unapata mbegu kutoka kwenye kampuni au wakala anayetambulika na aliyethibitishwa na mwenye leseni kutoka mamlaka husika.
Kuchagua mbegu za mahindi, zingatia yafuatayo;
- Chagua mbegu nzima ambazo hazijavunjika, kupondwa au kuharibika kwa aina yoyote
- Mbegu ziwe za viwango bora
- Ziwe zimekaushwa vizuri kufikia unyevunyevu wa 13%
- Ziwe za aina moja
- Safi, zisiwe zimechanganywa na uchafu, mawe au mbegu zingine
- Uwezo wa kuota uzidi 85%
- Ziwe mbegu zinazoweza kuota
- Ziwe mbegu ambazo hazijaathiriwa na magonjwa
- Mbegu zisichanganywe na mbegu za nyasi au magugu na mbegu za mazao mengine
- Ziwe mbegu ambazo zinaweza kuhimili magonjwa
- Ziwe mbegu zilizonunuliwa sehemu zilizothibitishwa au kuandaliwa na wewe mwenyewe kutoka kwenye mavuno ya msimu uliopita