Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kuvuna na Kuhifadhi

Sehemu hii tutajikita kuzungumzia; Kuvuna Mahindi Yaliyokauka, Maandalizi ya Kuvuna, Njia za Kuvuna, Kuhifadhi Mahindi, Teknolojia za kuhifadhi Mahindi, Faida za njia za Kisasa kuhifadhi Mahindi, Sifa za Chumba cha kuhifadhi Mahindi, Usafi wa Jumla katika Kuhifadhi, Wadudu katika kuhifadhi, Sumu ya Mycotoxins, na Njia Zingine za Kudhibiti Fangasi.

Kuvuna Mahindi Yaliyokauka

Mahindi yanavunwa yakiwa mabichi au yakiwa yamekauka. Sisi tutajikita kuzungumzia kuvuna mahindi yaliyokauka. Mahindi yanakuwa yamekauka na tayari kwa kuvuna ikiwa;

  • Majani mengi ya mmea yamekauka
  • Mhindi (wenye mahindi ndani) ukiwa sio wa kijani
  • Mmea wa mhindi kuanzia chini mpaka juu ukiwa wa njano au kahawia
  • Mhindi (wenye mahindi ndani) ukianza kama kudondoka kutoka kwenye mmea wa mhindi
  • Punje za mahindi zikionyesha utando mweusi kati ya mbegu na gunzi
  • Punje zikiwa ngumu na hazitoi majimaji ukiziminya
  • Mahindi yanapokuwa hayafai kuchomwa au kupikwa yakiwa kwenye gunzi