Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Uza na Kununua

Kuvuna na Kuhifadhi

Sehemu hii tutazungumzia; Kuvuna Mahindi Yaliyokauka, Maandalizi ya Kuvuna, Njia za Kuvuna, Kuhifadhi Mahindi, Teknolojia za kuhifadhi Mahindi, Faida za njia za Kisasa kuhifadhi Mahindi, Sifa za Chumba cha kuhifadhi Mahindi, Usafi wa Jumla katika Kuhifadhi, Wadudu katika kuhifadhi, Sumu ya Mycotoxins, na Njia Zingine za Kudhibiti Fangasi.

Sifa za Chumba cha kuhifadhi Mahindi

Chumba au jengo linalotumika kuhifadhi mahindi linapaswa;
  • Paa lake lisiwe linavuja
  • Sakafu isiwe yenye kupitisha maji au unyevunyevu na iwe katika hali nzuri na iwe rahisi kuisafisha
  • Ukuta uwe rahisi kusafishwa
  • Kusiwepo na matundu yanayoweza kupitisha, ndege, wanyama kama panya au wadudu kama mende
  • Kuwepo na hewa ya kutosha
  • Hushauriwi kutumia feni
Nyumba yenye paa lililoharibika na matundu Matumizi ya feni hayashauriwi