Sehemu hii tutazungumzia; Kuvuna Mahindi Yaliyokauka, Maandalizi ya Kuvuna, Njia za Kuvuna, Kuhifadhi Mahindi, Teknolojia za kuhifadhi Mahindi, Faida za njia za Kisasa kuhifadhi Mahindi, Sifa za Chumba cha kuhifadhi Mahindi, Usafi wa Jumla katika Kuhifadhi, Wadudu katika kuhifadhi, Sumu ya Mycotoxins, na Njia Zingine za Kudhibiti Fangasi.
Wadudu hatari katika kuhifadhi Mahindi
Baadhi ya wadudu wanaoshambulia mazao yakiwa yamehifadhiwa ni kama; Mchwa, Sitophilus spp., Sitotroga cerealella, Prostephanus truncates, Pyralid moths, na Gnatocerus.
Kudhibiti Wadudu
Wadudu wanaoshambulia mazao yaliyohifadhiwa wanaweza kudhibitiwa kwa kutumia kemikali na njia nyinginezo. Njia za kuhifadhi mazao zilizo boreshwa ambapo hewa na maji haviwezi kupita (hermetic) huweza kuwaua wadudu walio kwenye mazao maana watashindwa kupumua.
Kufukizia (Fumigation)
Hii njia hutumika kufukizia kemikali kwenye mazao yaliyohifadhiwa ili kudhibiti wadudu. Kemikali zinazotumika mara kwa mara ni hizi zifuatazo;
Phosphine 1,3-dichloropropene Chloropicrin Methyl isocyanate Hydrogen cyanide |
Sulfuryl fluoride Formaldehyde Iodoform Acrylonitrile Ethylene oxide |
Katika hizo zilizotajwa, Phosphine ndiyo hutumika zaidi kudhibiti wadudu wanaoshambulia mazao yaliyohifadhiwa. Tatizo ni kuwa ikitumika vibaya husababisha baadhi ya wadudu haribifu kutoathirika na hiyo kemikali.
Tahadhari: Kufukiza (Fumigation) ni hatari. Ni matakwa ya Kisheria kuwa anayefanya kazi ya kufukiza awe anatambulika na kusajiliwa na mamlaka husika za nchi kufanya kazi hiyo kwasababu kemikali hizo ni sumu kwa watu pamoja na wanyama wengineo.
Faida za Kufukiza (Fumigation)
Hasara za Kufukiza
Usalama wakati wa Kufukiza (angalia kemikali za shambani)