Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Uza na Kununua

Kuvuna na Kuhifadhi

Sehemu hii tutazungumzia; Kuvuna Mahindi Yaliyokauka, Maandalizi ya Kuvuna, Njia za Kuvuna, Kuhifadhi Mahindi, Teknolojia za kuhifadhi Mahindi, Faida za njia za Kisasa kuhifadhi Mahindi, Sifa za Chumba cha kuhifadhi Mahindi, Usafi wa Jumla katika Kuhifadhi, Wadudu katika kuhifadhi, Sumu ya Mycotoxins, na Njia Zingine za Kudhibiti Fangasi.

Maandalizi ya Kuvuna

Inabidi kuvuna mahindi baada ya maandalizi fulani kufanyika. Bila maandalizi mazuri itapelekea changamoto kadhaa ambazo zitasababisha kazi ya kuvuna isifanyike vizuri na mahindi yasihifadhiwe vizuri hivyo kuharibika na nk. Fanya yafuatayo kabla hujaanza kuvuna;
  • Vifaa vitakavyotumika kuvuna na baada ya kuvuna viandaliwe, viwe katika hali nzuri.
  • Andaa sehemu ya kukaushia na kupukuchulia mahindi.
  • Mahali yatakapohifadhiwa paandaliwe pia, viroba (mifuko/ magunia) viandaliwe na vyote visafishwe kabla ya mavuno mapya kuondoa mabaki ya msimu uliopita ili magonjwa na wadudu wa msimu uliopita visiambukize mazao mapya.
  • Mazao ya zamani yawekwe sehemu tofauti kwa matumizi yatakayopangwa.