Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kuvuna na Kuhifadhi

Sehemu hii tutazungumzia; Kuvuna Mahindi Yaliyokauka, Maandalizi ya Kuvuna, Njia za Kuvuna, Kuhifadhi Mahindi, Teknolojia za kuhifadhi Mahindi, Faida za njia za Kisasa kuhifadhi Mahindi, Sifa za Chumba cha kuhifadhi Mahindi, Usafi wa Jumla katika Kuhifadhi, Wadudu katika kuhifadhi, Sumu ya Mycotoxins, na Njia Zingine za Kudhibiti Fangasi.

Teknolojia za kuhifadhi Mahindi

Unaweza kutumia teknolojia za kiasili au za kisasa kuhifadhi mahindi. Baadhi ya njia hizo ni;
Teknolojia za Kiasili Teknolojia za Kisasa
  1. Vibanda vya mviringo vilivyotengenezwa kwa udongo na miti (hasa mianzi)
  2. Vikapu
  3. Vyungu
  4. Vikapu vya jute
  1. Visivyopitisha hewa na maji
    1. Tenki la PVC/ Silo
    2. Tenki la chuma/ Silo
    3. Mifuko ya Kokuni (Cocoon)
    4. Triple bagging
  2. Maghala

Kumbuka:

  1. Teknolojia za kiasili haziwezi kuhifadhi mahindi kwa kipindi kirefu ukilinganisha na teknolojia za kisasa
  2. Teknolojia isiyopitisha hewa na maji ni njia ya kisasa isiyopitisha hewa na unyevunyevu kati ya mazao (mahindi) na mazingira mahindi yalipohifadhiwa
  3. Njia itakayotumika izingatie pamoja na mambo mengine gharama za kuitumia, kiasi cha mahindi kinachotakiwa kuhifadhiwa, muda wa kuhifadhi mahindi na hali ya hewa kiujumla

Njia za asili na kawaida kuhifadhi mahindi Njia za kisasa (Silo) kuhifadhi mahindi. Silo ndogo huweza kutumika na kuwekwa ndani ya nyumba.