Kuvuna na Kuhifadhi
Sehemu hii tutazungumzia;
Kuvuna Mahindi Yaliyokauka,
Maandalizi ya Kuvuna,
Njia za Kuvuna,
Kuhifadhi Mahindi,
Teknolojia za kuhifadhi Mahindi,
Faida za njia za Kisasa kuhifadhi Mahindi,
Sifa za Chumba cha kuhifadhi Mahindi,
Usafi wa Jumla katika Kuhifadhi,
Wadudu katika kuhifadhi,
Sumu ya Mycotoxins, na
Njia Zingine za Kudhibiti Fangasi.
Njia za Kuvuna
Kwa wakulima wadodo wadogo mahindi yanavunwa kwa kunyofoa mhindi kutoka kwenye shina lake au kukata shina la mhindi na baadae kunyofoa mhindi.
Zingatia yafuatayo unapovuna mahindi;
- Vuna mahindi yakiwa tayari kuvunwa kwa matumizi husika (vuna katika muda sahihi)
- Usichelewe kuvuna mahindi maana mahindi yataharibika na kusababisha mavuno kidogo na yasiyo na ubora unaotakiwa
- Inafaa kuvuna mahindi yaliyokauka kipindi kisicho cha mvua maana unyevunyevu na maji husababisha mahindi kuharibika
- Hakikisha mahindi yaliyovunwa hayachafuliwi na udongo au mchanga au vitu vingine
 |
 |
Mahindi mabichi yaliyo tayari kuvunwa |
Kuvuna mahindi yaliyokauka |