Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kuvuna na Kuhifadhi

Sehemu hii tutazungumzia; Kuvuna Mahindi Yaliyokauka, Maandalizi ya Kuvuna, Njia za Kuvuna, Kuhifadhi Mahindi, Teknolojia za kuhifadhi Mahindi, Faida za njia za Kisasa kuhifadhi Mahindi, Sifa za Chumba cha kuhifadhi Mahindi, Usafi wa Jumla katika Kuhifadhi, Wadudu katika kuhifadhi, Sumu ya Mycotoxins, na Njia Zingine za Kudhibiti Fangasi.

Kuhifadhi Mahindi

Njia mbalimbali zinaweza kutumika kuhifadhi mahindi yaliyovunwa. lakini kabla ya kuhifadhi inabidi mahindi yawe yamekaushwa. Kwa mkulima mdogo, sehemu ya kuhifadhi mahindi yapasa;
  • Itengenezwe kwa zana na vifaa vinavyopatikana eneo lake
  • Izuie mahindi kushambuliwa na mchwa, panya, na wadudu na wanyama wengine
  • Izuie mvua isinyeshee mahindi
  • Isihitaji ujuzi mkubwa kuitengeneza na kuikarabati

Lengo la Kuhifadhi Mahindi
Lengo kuu la kuhifadhi mahindi ni kuyafanya mahindi;

  • Yasiathiriwe na maji ya mvua au yatokayo chini ya ardhi na unyevunyevu
  • Yasiharibiwe na wadudu na wanyama
  • Yasiathiriwe na joto kali

Kabla ya Kuhifadhi Mahindi

Inatakiwa mahindi yakaushwe kwanza kabla ya kuhifadhiwa;
Usianike Chini Anika kwenye turubai

Waangalie na wasikilize wataalamu, hapa wanazungumzia baadhi ya vitu vya kufanya kabla ya kuhifadhi mahindi (Video)