Mbegu na Kupanda
Sehemu hii tutazungumzia;
madaraja ya mbegu na faida za matumizi ya mbegu bora,
kuchagua mbegu bora,
kuangalia uotaji wa mbegu,
muda wa kupanda,
kina cha mashimo,
na jinsi ya kupanda.
Kuangalia Uotaji wa Mbegu
Ni muhimu kuwa na uhakika na uotoja wa mbegu zako. Kufanya hivyo fanya yafuatayo;
- Wiki moja kabla hujapanda shambani, chukua punje za mahindi (mbegu) 100 bila mpangilio maalumu
- Weka hizo mbegu kwenye boksi pamoja na mchanga. Toboa hilo boksi chini ili kuruhusu maji kuweza kupungua
- Zifanye mbegu kuwa na unyevunyevu, lakini zisiwe kwenye maji. Maji mengi sana au pungufu sana huweza kufanya mbegu zisiote
- Baada ya siku 7, taratibu chimbua mbegu kutokw kwenye mchanga, ziweke kwenye karatasi na hesabu miche kwenye kila kundi
- Miche ya kawaida – mizizi, shina na majani vimekua vizuri
- Isiyo ya kawaida – ina dalili kati ya zifuatazo: hamna mizizi, mizizi dhaifu, hamna majani, majani dhaifu
- Imeoza, ina magonjwa na mbegu ambazo hazijaota
Kundi |
Idadi ya mbegu |
Zimeota kawaida |
Isiyo ya kawaida |
Imeoza, ina magonjwa, hazipo |
Boksi la kwanza |
100 |
X |
Y |
Z |
- Kama kuota ni chini ya 90% lakini juu ya 85%, ongeza idadi ya mbegu utakazopanda kwenye ekari moja kwa kufuata hesabu hapa chini;
- Kawaida unashauriwa kupanda Kg10 kwenye ekari moja
- Asilimia ya kuota ni 85%
- Kurekebisha kupanda kwenye ekari = (100 / 85) * Kg10 = Kg12
- Sasa unashauriwa kupanda Kg12 kwenye ekari moja badala ya Kg10 kwenye ekari moja kwasababu kuna mbegu hazitaota
- Kama kiasi cha kuota ni chini ya asilimia 85%, hizo mbegu hazifai achana nazo
- Toa taarifa kwa bwana shamba na/ au kwa aliyekuuzia hizo mbegu juu ya jambo hili