Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Maandalizi ya Shamba

Katika sehemu hii tutazungumzia; kazi katika kuandaa shamba, matumizi ya moto, njia za kulima na zana za kulimia, mahitaji ya mahindi (udongo unaofaa na hali ya hewa inayofaa) na vitu vinavyosababisha rutuba kupotea kutoka kwenye shamba.

Njia za Kulima na Zana za Kulimia

Shamba la kupanda mahindi linaweza kulimwa kwa njia za kawaida za ulimaji au kwa kutumia njia ambazo zina lenga kuhifadhi mazingira.

Njia za Kawaida

Mkulima anatumia zana kama jembe la mkono, jembe la kukokotwa na ng’ombe au wanyama wengine (plau), au trekta la mkono.
  • Jembe la mkono ndilo linatumika na wakulima wengi wadogowadogo lakini kazi ya kulima inafanyika polepole na linahitaji nguvu nyingi za mwili
  • Jembe la kukokotwa na ng’ombe au wanyama wengine huwa halifai kwenye udongo mzito na kwenye miteremko. Hii njia inafaa zaidi, gharama sio kubwa sana, ni ya uhakika na imethibitishwa kwamba ni teknolojia inayoweza kuwafaa wakulima wadogowadogo na wakati
  • Njia ya kutumia matrekta ni ghali zaidi mara ingine (sio mara zote) na hutumika zaidi kwa kilimo cha kibiashara
  • Matrekta ya mkono (power tiller) hutumika na wakulima wadogowadogo na wa kati
Jembe la mkono Plau (jembe) la kukokotwa na wanyama kama ng'ombe
Matumizi ya Pawatila Matumizi ya Trekta

Kulima kwa Kuhifadhi Mazingira

Katika kilimo hiki udongo wa shambani haulimwi sana na pia hulimwa mara chache ili kuhifadhi mazingira. Lengo kuu ni kutengeneza mazingira ambayo zao husika litastawi lakini pia maji, udongo na virutubisho vingine vya udongo vitabaki katika hali yake ya awali kwa kupunguza kuusumbua udongo na kubakiza mabaki ya mimea shambani.
  • Njia hizi hubakiza mabaki ya nyasi na mimea katika 30% ya shamba baada ya kulima
  • Katika kilimo hiki matumizi ya madawa ya kuua nyasi na mimea isiyotakiwa shambani kama Glyphosate ni muhimu sana
  • Kuendesha kilimo hiki, kwanza ondoa visiki na vitu vingine visivyotakiwa shambani
  • Kama shamba lina vichaka na nyasi nyingi vikate na subiria nyasi ziote halafu nyunyizia madawa ya kuua nyasi na mimea isiyotakiwa shambani kama Round-up, Weedmaster, mamba au Weedall
  • Kina kinachofaa cha kupandia mbegu kizingatiwe maana udongo unakuwa haujalainishwa kiasi cha kutosha hivyo mbegu zitahitaji nguvu zaidi kuweza kupenyeza mizizi ardhini