Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Uza na Kununua

Maandalizi ya Shamba

Katika sehemu hii tutazungumzia; kazi katika kuandaa shamba, matumizi ya moto, njia za kulima na zana za kulimia, mahitaji ya mahindi (udongo unaofaa na hali ya hewa inayofaa) na vitu vinavyosababisha rutuba kupotea kutoka kwenye shamba.

Vitu vinavyosababisha rutuba Kupotea

Tunasema shamba halina rutuba kwa kilimo cha zao fulani kama udongo wa hilo shamba hauna sifa za kuuwezesha mmea kupata virutubisho vinavyotakiwa kwa kiwango sahihi kuuwezesha kuota na kustawi. Rutuba (virutubisho) katika udongo huongezeka tunapoweka mbolea za asili au za viwandani. Virutubisho hivyo hupotea au hupungua kupitia njia zifuatazo;

  • Tunapovuna mazao
  • Kukitokea mmomonyoko wa udongo
  • Majanga kama mafuriko na moto unaounguza misitu
  • Kuondoa mabaki ya mazao shambani
  • Kuchoma moto mabaki ya mazao shambani na kuharibu mimea mingine shambani
  • Hali mbaya ya udongo kama vile kutoweza kupenyezesha maji inavyotakiwa na pale mizizi ya mimea inaposhindwa kupenya kwende udongo kunakosababishwa na mshikamano mkubwa wa udongo
  • Kupotea kwa virutubisho katika udongo kunakosababishwa na mvua au umwagiliaji
  • Asidi inapokuwa ndogo sana katika udongo au inapokuwa nyingi sana. Au Alkali inapokuwa ndogo sana au kuwa nyingi sana
  • Matumizi ya muda mrefu ya mbolea za viwandani (huongeza sana kiwango cha tindikali katika udongo)

Mmomonyoko wa udongo Mafuriko huweza kuondoa rutuba kutoka sehemu moja kwenda ingine
Kuvuna na pia kuvuna na kuondoa mabaki ya mavuno shambani Kuchoma mabaki ya mavuno