Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Nyasi na magugu ya kila mwaka (annual weeds)
Hukamilisha mzunguko wake ndani ya msimu mmoja. Mara nyingi, mbegu za aina hii ya nyasi na magugu huota haraka na mmea wake kukua haraka kuliko mahindi. Hizi nyasi na magugu huathiri ukuaji wa mwanzo wa mahindi. Na huzalisha mbegu zingine nyingi zitakazo dumu na kuota tena msimu ujao. Baadhi ya mbegu za hizi nyasi na magugu husambaa kwa njia ya upepo, maji, watu, zana za kilimo an mbedu za mazao zilizochanganyikana na uchafu au vitu vingine.
Nyasi na magugu ya kudumu (perennial weeds)
Nyasi na magugu ya msimu kwa msimu
Haya magugu hudumu kwenye shamba la mahindi muda wote kila mwaka na huzaliana kupitia mizizi na mashina. Ni vigumu kuyadhibiti hii mimea kwa kutumia mashine maana ukifanya hivyo utakata sehemu ya juu tu na mizizi yake itabaki kuendelea kuathiri mahindi kwa kunyonya virutubisho na maji.
Kudhibiti hizi nyasi na magugu inabidi ufanye hivyo kabla ya msimu wa kupanda kwa kuondoa mashina na mizizi ya hizi nyasi na magugu. Mfano ni couch grass, spear grass etc.