Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Faida za matumizi ya kemikali kudhibiti nyasi na magugu

Kuna faida nyingi za kutumia kemikali shambani ili kuondoa nyasi na magugu. Baadhi ya faida ni;
  • Hizi kemikali zinafanya kazi kwa usahihi zaidi na huchukua muda mfupi matokeo yake kuonekana
  • Hupunguza kiasi cha ulimaji wa shamba na hivyo hupunguza kazi ya kulima
  • Mizizi ya mahindi haiathiriwi na udongo hausumbuliwi
  • Ni lazima kutumia kemikali hizi kama unataka kuendesha kilimo cha kuhifadhi mazingira

Unapotumia kemikali shambani zingatia yafuatayo

  • Usipotumia kemikali sahihi matokeo yake yatakuwa mabaya sana.
  • Pia usipotumia kiwango sahihi matokeo yake yatakuwa mabaya.
  • Kemikali hizi ni ghali sana na ni sumu kwa mtumaji kama hazitatumika inavyopasa.
  • Vaa mavazi rasmi yanayotakiwa unapotumia kemikali hizi shambani

Juu ya Nyasi na magugu shambani soma pia; Aina za nyasi na magugu, Matatizo yasababishwayo na nyasi na magugu, Njia za kuzuia nyasi na magugu, Njia za kuondoa nyasi na magugu shambani, Faida za matumizi ya kemikali kudhibiti nyasi na magugu, na Visababishi vya magonjwa na wadudu hatari.