Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Njia za kuzuia nyasi na magugu

Utapunguza uwezekano wa shamba lako kuwa na nyasi na magugu kwa kufanya haya yafuatayo;
  • Lima shamba vizuri kabla ya kupanda
  • Wakati wa kupanda, ondoa nyasi na magugu na wakati wa palizi zungushia udongo kwenye mashina ya miche ya mahindi
  • Kila inapowezekana ng’oa nyasi na magugu na mizizi yake
  • Ng’oa nyasi angalau wiki 3 baada ya mahindi kuota na urudie kung’oa nyasi baada ya mahindi kufikia kimo cha magoti
  • Panda mazao jamii ya kunde (kama maharage) ili yazuie kuota kwa nyasi shambani

Juu ya Nyasi na magugu shambani soma pia; Aina za nyasi na magugu, Matatizo yasababishwayo na nyasi na magugu, Njia za kuzuia nyasi na magugu, Njia za kuondoa nyasi na magugu shambani, Faida za matumizi ya kemikali kudhibiti nyasi na magugu, na Visababishi vya magonjwa na wadudu hatari.