Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Shamba lililopaliliwa kwa jembe la mkono | Njia ya kutumia kemikali kuua nyasi na magugu shambani |
Kukinga na Njia za Kiasili
Hizi ni njia ambazo zikitumika zitafanya shamba lisiwe katika uwezekano mkubwa wa nyasi au magugu kuota au kuongezeka shambani. Hizi ni kama zifuatazo;
Kutumia zana rahisi za Kilimo
Hii inahusisha matumizi ya vifaa na zana kama majembe ya mikono, reki, mapanga na nk.
Inabidi kuwa makini ili kuondoa uwezekano wa kuharibu mimea ya mazao yaliyopandwa.
Angalia Palizi kwa mikono na jembe la mikono (Video)
Kutumia Mashine Kubwa
Hii inahusisha matumizi ya viifaa kama jembe linalovutwa na ng’ombe, trekta la kung’oa nyasi na magugu.
Ili njia hizi ziweze kutumika inabidi mahindi yawe yamepandwa kwenye mistari na upaliliaji wa njia hii hufanyika mahindi yakifikia ukuaji fulani.
Matumizi ya Kemikali
Njia hii ama huongeza kasi, husimamisha, au hubadilisha ukuaji wa kawaida wa nyasi au magugu shambani. Matokeo yake majani, mashina na mizizi ya nyasi na magugu hukauka.
Kemikali za kudhibiti nyasi na magugu shambani zinafanya kazi vizuri sana zikitumika vyema. Mkulima inapaswa afahamu aina, kiasi sahihi na wakati gani wa umri wa mahindi hizi kemikali zitumike.
Tahadhari zote za usalama zinatakiwa kufuatwa na lebo za maelekezo lazima zifuatwe kama zilivyoandikwa.