Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Visababishi vya magonjwa na wadudu hatari

Baadhi ya vitu vinavyosababisha magonjwa na wadudu hatari kwenye shamba la mahindi ni pamoja na;
  • Matumizi ya samadi shambani ambayo haijaoza vizuri
  • Mabaki ya mazao ya msimu uliopita kama hayakuoza vizuri
  • Kama shamba halikusafishwa vizuri
  • Nyasi na magugu zinazokaribiana na mazao shambani, wekea mpaka wa kutosha kati ya shamba lako na sehemu ambayo haijapandwa mazao
  • Kuna fangasi kama Downey mildew wanaweza kuathiri mahindi kama hali ya joto na unyevunyevu viko juu
  • Mbegu zisizo na ubora unaotakiwa

Juu ya Nyasi na magugu shambani soma pia; Aina za nyasi na magugu, Matatizo yasababishwayo na nyasi na magugu, Njia za kuzuia nyasi na magugu, Njia za kuondoa nyasi na magugu shambani, Faida za matumizi ya kemikali kudhibiti nyasi na magugu, na Visababishi vya magonjwa na wadudu hatari.