Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Matatizo yasababishwayo na nyasi na magugu
Nyasi na magugu shambani ni kikwazo kikubwa kwa uzalishaji wa mazao shambani. Tafiti zinaonyesha nyasi na magugu huongeza gharama kwa mkulima na kupunguza uzalishaji kuliko wadudu waharibifu shambani.
- Nyasi na magugu shambani hugombania virutubisho, maji na unyevunyevu, hewa, nafasi na mwanga na mazao
- Baadhi ya nyasi na magugu ni sehemu ya wadudu wabaya na magonjwa kujihifadhi
- Baadhi ya nyasi na magugu huchukua virutubisho kutoka kwenye mimea ya mahindi
- Baadhi ya nyasi na magugu hutoa sumu inayoathiri ukuaji wa mahindi
- Nusu au zaidi ya mavuno ya mahindi yanaweza kupotea kama hutopalilia vizuri shamba
- Mimea ya mahindi inatakiwa itangulie kuota shambani kabla ya nyasi na magugu
- Baada ya mahindi kuchipua shamba la mahindi halitakiwi kuwa na nyasi na magugu angalau kwa wiki 10 za mwanzo
- Hakikisha nyasi na magugu shambani havikui mpaka kutoa mbegu maana itasababisha shamba kuwa na nyasi na magugu mengi hapo baadae (misimu ijayo)
- Nyasi na magugu hufanya kazi ya uvunaji wa mahindi kuwa ngumu
Juu ya Nyasi na magugu shambani soma pia;
Aina za nyasi na magugu,
Matatizo yasababishwayo na nyasi na magugu,
Njia za kuzuia nyasi na magugu,
Njia za kuondoa nyasi na magugu shambani,
Faida za matumizi ya kemikali kudhibiti nyasi na magugu, na
Visababishi vya magonjwa na wadudu hatari.