Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Kilimo hiki kinaweza endeshwa kama ifuatavyo: Mwaka wa kwanza panda mahindi. Mwaka unaofuata liache shamba bila kulilima. Mwaka wa tatu panda maharage ya soya. Mwaka wa nne panda mahindi kama ulivyopanda mwaka wa kwanza. Mwaka wa pili badala ya kuliacha shamba bila kulipanda unaweza kupanda mazao ya mizizi kama vile viazi.
Kama mkulima hawezi kuacha mwaka mzima bila kulima mahindi au maharage, inabidi shamba lake aligawanye sehemu tatu(3) au uwe na mashamba matatu (3).Juu ya Mbolea (virutubisho) shambani pia soma; Mambo muhimu kuhusu mbolea, Kujua uhitaji wa mbolea, Virutubisho vikuu na virutubisho vidogovidogo, Mambo ya kuzingatia kuhusu mbolea, Matumizi ya mbolea za asili, na Kilimo mzunguko.