Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Mambo ya kuzingatia kuhusu mbolea
Zingatia yafuatayo kuhusu mbolea;
- Matumizi sahihi ya mbolea shambani huongeza rutuba kwenye shamba
- Shamba lenye rutuba inayofaa kwa kilimo cha zao fulani hutoa mazao mengi na bora
- Mmea wa mahindi hupitia hatua mablimbali za ukuaji mpaka kuvunwa na katika kila hatua huhitaji kiasi/ kiwango tofauti cha virutubisho hivyo inatakiwa mbolea kuwekwa kiwango/ kiasi sahihi katika wakati sahihi wa ukuaji wake
- Mbolea tofauti zana viwango tofauti vya virutubisho. Baadhi ya virutibisho vya mahindi vilivyo kwenye mbole ni kama; Nitrogen, Phosphorus, Potassium, Magnesium, Calcium, Sulfur, Boron, Copper, Iron, Manganese na Zinc
- Zao la mahindi huhitaji kiwango kikubwa zaidi cha Nitrogen, Phosphorus, na Potassium
- Kukosekana kwa moja ya virutubisho hivyo tajwa husababisha mmea wa mahindi kuonyesha dalili fulani na kama virutubisho havitaongezwa mkulima hatopata mazao mengi na bora
- Virutubisho vya mmea wa mahindi huweza kupatikana kwenye udongo wa shamba lenyewe, mbolea za asili au mbolea za viwandani
Juu ya Mbolea (virutubisho) shambani pia soma;
Mambo muhimu kuhusu mbolea,
Kujua uhitaji wa mbolea,
Virutubisho vikuu na virutubisho vidogovidogo,
Mambo ya kuzingatia kuhusu mbolea,
Matumizi ya mbolea za asili, na
Kilimo mzunguko.