Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Mambo muhimu kuhusu mbolea

Kumbuka yafuatayo kuhusu zao la mahindi na mbolea/ virutibisho;
  • Mahindi ni miongoni mwa mazao yanayoongoza kwa kuhitaji kulimwa kwenye shamba lenye virutubisho vya kutosha
  • Kuna baadhi ya maeneo mahitaji ya mbolea kwenye shamba la mahindi ni makubwa kuliko mahitaji ya mbolea kwenye shamba la zao lolote linalolimwa kwenye eneo hilo
  • Kama udongo wa shamba lako hauna rutuba (virutubisho) ya kutosha hutoweza kupata mavuno ya kutosha hata kama utafuata njia bora kabisa za kilimo, mpaka utumie mbolea za viwandani au za asili au kuendesha kilimo mzunguko na mazao mengine ya jamii ya kunde
  • Kimsimgi kila unapovuna mahindi kwenye shamba lako unapunguza Nitrogen, Phosphate, Potassium na virutubisho vingine kutoka shambani
  • Unapunguza virutubisho vingi shambani unapovuna mmea mzima (silage) kwa matumizi ya malisho ya mifugo kuliko unapovuna mahindi ya kula binadamu (mbegu)

Angalia mtaalamu hapa anazungumzia mambo muhimu yahusuyo mbolea (Video)

Juu ya Mbolea (virutubisho) shambani pia soma; Mambo muhimu kuhusu mbolea, Kujua uhitaji wa mbolea, Virutubisho vikuu na virutubisho vidogovidogo, Mambo ya kuzingatia kuhusu mbolea, Matumizi ya mbolea za asili, na Kilimo mzunguko.