Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Matumizi ya mbolea za asili

Zingatia yafuatayo kuhusu mbolea za asili;
  • Mbolea za asili (za mimea iliyooza au samadi au vyote) viwekwe mapema baada ya kulima kwa mara ya kwanza ili viweze kuozea vizuri shambani. Unapolima mara ya pili hiyo mbolea inachanganywa zaidi na udongo kabla hujapanda. Hii mbolea iwekwe tani 4 – 6 kwa ekari moja
  • Kama unaendesha kilimo cha kuhifadhi mazingira, weka mbolea hii kwenye mashimo ambamo utapanda mahindi

Juu ya Mbolea (virutubisho) shambani pia soma; Mambo muhimu kuhusu mbolea, Kujua uhitaji wa mbolea, Virutubisho vikuu na virutubisho vidogovidogo, Mambo ya kuzingatia kuhusu mbolea, Matumizi ya mbolea za asili, na Kilimo mzunguko.