Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Kujua uhitaji wa mbolea

Utajua mbolea ya kutumia kwenye shamba kwa kufanya moja au zaidi katika haya;
  • Kupima udongo
  • Habari za utafiti kwa eneo husika
  • Majaribio yaliyokwishafanyika kwenye shamba husika
  • Virutubisho vilivyoondolewa au kupungua kwenye shamba husika
  • Uchambuzi / kuusoma au kuuchunguza (analysis) mmea au mimea kwenye shamba husika, na
  • Uzoefu wa siku za nyuma
Mbolea zina virutubisho vinavyotakiwa katika uotaji na ukuaji wote wa mmea. Upungufu wa moja kati ya hivi virutubisho utasababisha ukuaji wenye mapungufu katika mmea, kuathiri utoaji wa maua na kutengenezeka kwa mbegu. Virutubisho muhimu vya mahindi vinagawanyika katika makundi makuu mawili – virutubisho vikuu (macro nutrients) na virutubisho vidogovidogo (micro nutrients).

Msikilize mtaalamu hapa anazumgumzia juu ya mbolea ya kukuzia mahindi (Video)

Juu ya Mbolea (virutubisho) shambani pia soma; Mambo muhimu kuhusu mbolea, Kujua uhitaji wa mbolea, Virutubisho vikuu na virutubisho vidogovidogo, Mambo ya kuzingatia kuhusu mbolea, Matumizi ya mbolea za asili, na Kilimo mzunguko.