Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Virutubisho Vikuu (Macro-nutrients)
Hivi ni virutubisho vinavyotakiwa na mmea katika kiwango kikubwa. Hivi ni: Nitrogen, Phosphorus, Potassium, Sulfur, Calcium na Magnesium kwa upande wa mahindi.
Virutubisho vidogovidogo (Micro-nutrients)
Hivi ni virutubisho vinavyohitajika katika kiwango kidogo na mahindi. Hivi ni kama: Manganese, Iron, Boron, Zinc, Copper, Molybdenum, na nk.