Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Kabla ya kupulizia/ kunyunyizia
Kabla ya kupulizia (kunyunyizia) kemikali kwenye shamba lako, kumbuka yafuatayo;
- Kabla ya kunyunyizia angalia pampu yako ya kunyunyizia kama kuna sehemu inavuja.
- Tumia nozo (nozzle) sahihi kwa kazi sahihi. Mfano, nozo ambayo ni flat ni kwa ajili ya kemikali za kuua nyasi na magugu, nozo ambayo ni koni (cone) ni kwa ajili ya kunyunyizia kemikali za fangasi (fungicides) na wadudu (insecticides).
- Angalia kama nozo yako imejiziba. Kama imejiziba usijaribu kuizibua kwa kupuliza na mdomo, badala yake tumia nyasi au brashi kuizibua.
- Vaa mavazi rasmi kwa kazi ya kupulizia kemikali (kulinda pua, mwili, mikono, miguu na nk.) kama ilivyoshauriwa kwenye maelekezo ya kemikali.
Angalia video hapa chini zinazoelezea mambo muhimu kuhusu mavazi ya kupulizia madawa shambani na bomba la kupulizia na kuchanganya dawa;
Juu ya matumizi ya kemikali shambani soma pia
Magonjwa ya mahindi,
Makundi na faida za kemikali za Kilimo,
Matumizi salama ya kemikali za Kilimo,
Kuweka kemikali za Kilimo shambani,
Kuchanganya kemikali za Kilimo,
Kabla ya kupulizia,
Wakati wa kupulizia,
Baada ya kupulizia,
Kutupa makopo ya Kemikali, na
Kujisafisha mwenyewe na chombo cha kupulizia.