Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Kuweka kemikali za kilimo shambani
Fuata yafuatayo ili uweze kufanikisha hili kwa usahihi;
- Soma lebo (maelekezo)
Lebo ina maelekezo ya muhimu kama vile, jinsi ya kuchanganya, kiasi cha kuweka, msaada wa kwanza kukitokea shida, jinsi ya kutupa kopo/ kontena lenye dawa, na nk. Fuata maelekezo inavyotakiwa. Kama kuna kitu huelewi au huna uhakika nacho omba ushauri au msaada kutoka kwa Afisa wa Kilimo.
Vaa mavazi ya kujikinga na sumu kama inavyoshauriwa kwenye kopo au kontena la kemikali mfano, kofia, ovaroli, magwata (gumboots), kinga za mikono (gloves), miwani (goggles).
Angalia rangi, waranti, na maelekezo mengine yaliyowekwa kwenye lebo ya kemikali. Kuna rangi mbalimbali unaweza kuziona ambazo zinaelezea kiasi cha sumu katika kemikali.
Daraja Ia |
NYEKUNDU - C |
Sumu Kali Sana |
Daraja Ib |
NYEKUNDU - C |
Sumu Kali |
Daraja II |
NJANO - C |
Sumu |
Daraja III |
BLUU 293 - C |
Sumu Kidogo |
Daraja IV |
KIJANI 317 - C |
Chukua Tahadhari |
Kasi cha kemikali cha kuweka
Fuata yafuatayo ili uweze kufanikisha hili kwa usahihi;
- Amua kiasi cha kutumia cha kemikali
Swali moja la mara kwa mara linaloulizwa ni hili: “Niweke kiasi gani cha kemikali (ml) kwenye dumu la kupulizia (Lita 20)?” Jibu ni hili; inategemeana na vipimo kwenye dumu lako la kupulizia. Kwa ufupi, square mita ngapi pump moja ya maji iliyochanganywa na kemikali itamaliza.
Hakikisha umesoma kwenye maelekezo kiasic ha kuchanganya kemikali na maji.
Ukizidisha kemikali katika maji unaweza sababisha yafuatayo;
- Kupoteza kemikali ambayo ungeweza kuitumia sehemu ingine au msimu mwingine
- Kuharibika kwa mazao
- Kuchafuliwa na kuharibika kwa mazingira
Ukiweka kemikali kidogo katika maji unaweza kusababisha yafuatayo;
- Wadudu haribifu hawatodhurika na hivyo mazao yatazidi kuathirika
- Wadudu wanaweza kujitengenezea kinga dhidi ya hiyo kemikali na hivyo kutoathirika utakapokuja kuweka hapo baadae
Juu ya matumizi ya kemikali shambani soma pia Magonjwa ya mahindi, Makundi na faida za kemikali za Kilimo,
Matumizi salama ya kemikali za Kilimo,
Kuweka kemikali za Kilimo shambani,
Kuchanganya kemikali za Kilimo,
Kabla ya kupulizia,
Wakati wa kupulizia,
Baada ya kupulizia,
Kutupa makopo ya Kemikali, na
Kujisafisha mwenyewe na chombo cha kupulizia.