Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Kuchanganya kemikali za kilimo
Ajali nyingi za kemikali za Kilimo hutokea wakati wa kuchanganya na kujaza kemikali. Zingatia yafuatayo;
- Soma lebo kwa umakini na hakikisha umeelewa maelekezo
- Hakikisha viwango vya kemikali na maji kuchanganywa vimefuatwa
- Hakikisha kuchanganya na kujaza kunafanyika nje ya nyumba ili kuepuka uwezekano wa mvuke/ moshi/ harufu/ gesi kujikusanya kwenye eneo moja dogo lililofungwa
- Fungua kontena/ kopo la kemikali kwa umakini sana
- Kukitokea kuvuja kwa kemikali haraka osha hiyo sehemu na maji safi
- Tumia maji safi kuchanganyia na kemikali
- Tumia vifaa vinavyostahili kupimia kemikali
- Usitumie mikono kama kichanganyio cha kemikali na maji
- Weka kiasi cha kutosha tu cha kemikali kwenye dumu kinachoendana na ukubwa wa shamba unaloenda kulifanyia kazi
Juu ya matumizi ya kemikali shambani soma pia Magonjwa ya mahindi, Makundi na faida za kemikali za Kilimo,
Matumizi salama ya kemikali za Kilimo,
Kuweka kemikali za Kilimo shambani,
Kuchanganya kemikali za Kilimo,
Kabla ya kupulizia,
Wakati wa kupulizia,
Baada ya kupulizia,
Kutupa makopo ya Kemikali, na
Kujisafisha mwenyewe na chombo cha kupulizia.