Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Faida na makundi ya kemikali za kilimo

Kiujumla matumizi ya kemikali kuendesha kilimo kuna faida kadhaa, miongoni mwa hizo ni;
  • Uzalishaji unaongezeka na hivyo mkulima anapata faida
  • Husaidia kupatikana kwa mazao yenye ubora wa juu
  • Inapunguza gharama za uzalishaji, mfano matumizi ya kemikali za kuua nyasi na magugu
  • Inapunguza kiasi cha kazi kinachotakiwa kufanywa shambani
Kemikali za kilimo zinaweza zikagawanywa katika makundi makuu yafuatayo;
  • Kemikali za kuua nyasi na magugu (herbicides)
  • Kemikali za kuua wadudu (insecticides)
  • Kemikali za kudhibiti fangasi (fungicides)
  • Kemikali za kuua minyoo ya ardhini (nematicides)
  • Kemikali za kudhibiti panya na wanyama wengine waharibifu (rodenticides)
  • Mbolea (fertilizers) (hapa hatutagusia mbolea)

Athari za kemikali za kilimo

Kemikali za Kilimo zisipotumiwa vizuri huleta madhara mengi na makubwa kwa mtumiaji (mkulima), atakayekula hayo mazao na kwa mazingira. Baadhi ya matokeo mabaya ya matumizi mabaya ya kemikali za Kilimo ni pamoja na;
  • Kuharisha
  • Kuumwa tumbo
  • Kuvuja damu puani
  • Kutapika
  • Kupata upofu
  • Kusinzia
  • Kifo
Athari za kimazingira ni kama vile;
  • Kuchafuliwa kwa mito, na maziwa
  • Kuchafuliwa na kuharibika kwa mashamba
  • Kuumwa au kufa kwa ndege, wanyama

Juu ya matumizi ya kemikali shambani soma pia Magonjwa ya mahindi, Makundi na faida za kemikali za Kilimo, Matumizi salama ya kemikali za Kilimo, Kuweka kemikali za Kilimo shambani, Kuchanganya kemikali za Kilimo, Kabla ya kupulizia, Wakati wa kupulizia, Baada ya kupulizia, Kutupa makopo ya Kemikali, na Kujisafisha mwenyewe na chombo cha kupulizia.

<