Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Wakati wa kupulizia/ kunyunyizia
Wakati wa kupulizia zingatia yafuatayo;
- Weka alama za tahadhari kwenye shamba au eneo husika kuwa tahadharisha watu
- Usipulizie kemikali za Kilimo karibu na watu au karibu na maji au chanzo cha maji
- Pulizia kuelekea upepo unakoelekea
- Pita kwenye mistari na elekeza tundu la kutoloea dawa (nozzle) kwenye wadudu wanaolengwa
- Inafaa zaidi kupulizia nyakati za asubuhi kabla ya saa tano au jioni baada ya saa kumi ambapo muda huo wadudu wanakuwa na nguvu zaidi
- Usipulizie wakati mvua inakaribia kunyesha au wakati mvua inanyesha
- Usile, kunywa au kuvuta sigara au tumbaku au chochote wakati unapofanya kazi na kemikali za Kilimo
- Punguza kuongea wakati unapulizia au kufanya kazi na kemikali za Kilimo
- Usiguse uso au sehemu ingine ya mwili wako na mikono yenye kemikali au glovu zenye kemikali
- Pulizia au nyunyizia kemikali kwa kiasi na kiwango sawa sehemu zote
- Zima kifaa chako wakati unapopumzika au ukimaliza
- Tumia kemikali yote kupulizia shambani, na kama imebaki pulizia kwenye mashamba au hata nyasi za pembeni ya shamba
- Ikitokea sumu imekuingia au imemuingia mwenzio simamisha zoezi la kupulizia au kunyunyizia kemikali mara moja na jipatie au upatiwe au mpatie mwenzio huduma ya kwanza haraka
Juu ya matumizi ya kemikali shambani soma pia Magonjwa ya mahindi, Makundi na faida za kemikali za Kilimo,
Matumizi salama ya kemikali za Kilimo,
Kuweka kemikali za Kilimo shambani,
Kuchanganya kemikali za Kilimo,
Kabla ya kupulizia,
Wakati wa kupulizia,
Baada ya kupulizia,
Kutupa makopo ya Kemikali, na
Kujisafisha mwenyewe na chombo cha kupulizia.