Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Kutupa makopo ya kemikali

Makopo au madumu uliyonunulia kemikali za shambani inafaa yatupwe kiuangalifu. Fanya yafuatayo;
  • Suuza na maji angalau mara tatu (3)
  • Kama chombo kimetengenezwa na chuma, kitoboe na kama kimetengenezwa na plastic fanya hivyohivyo au kikate mara kadhaa kuepusha kuokotwa na watu au watoto na kutumiwa kwa matumizi mengine
  • Chagua sehemu ya kutupa mbali na makazi ya watu na kitupe huko
  • Weka au andika tahadhari kwenye chombo ulichotupa ukizingatia tahadhari zilizokuwa kwenye lebo wakati unanunua

Juu ya matumizi ya kemikali shambani soma pia Magonjwa ya mahindi, Makundi na faida za kemikali za Kilimo, Matumizi salama ya kemikali za Kilimo, Kuweka kemikali za Kilimo shambani, Kuchanganya kemikali za Kilimo, Kabla ya kupulizia, Wakati wa kupulizia, Baada ya kupulizia, Kutupa makopo ya Kemikali, na Kujisafisha mwenyewe na chombo cha kupulizia.