Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Matumizi salama ya kemikali za kilimo

Ili uweze kuzitumia kiusahihi na kiusalama kemikali za Kilimo ni muhimu kutambua tatizo lililoko shambani kwako kwanza ambalo litahitaji matumizi ya hizo kemikali shambani. Fanya yafuatayo;
  1. Utambuzi wa mdudu mharibifu
    • Anza kwa kumtambua mdudu au wadudu waharibifu walioko shambani kwako na kiwango cha uharibifu au maambukizi katika mazao yako. Ukiwa na wasiwasi, wasiliana na Afisa wa Kilimo au chukua baadhi ya mimea iliyoathirika (michache sana) na uipeleke kwa mtaalamu wa Kilimo aliyethibitishwa kwa ushauri.
  2. Kununua kemikali za Kilimo
    • Mara zote nunua kemikali za Kilimo kutoka kwenye duka au kwa mtu aliyesajiliwa na kuthibitishwa na mamlaka husika.
    • Soma lebo iliyobandikwa kwenye hiyo kemikali, mfano tarehe ya mwisho wa matumizi na nk.
    • Mara zote nunua dawa za kuua wadudu zikiwa kwenye vifungashio vyake vya mwanzo toka ilikotengenezwa na hakikisha hivyo vifungashio havijafunguliwa
    • Hakikisha hiyo kemikali sio feki
    • Muuzaji akupe risiti ya ulichonunua ikiwa na habari muhimu mfano, tarehe ya kununua, bei, jina la kemikali na nk.
  3. Kusafirisha kemikali za Kilimo
    • Hakikisha kifungashio cha kemikali kimefungwa vizuri na utakapokuwa una safirisha hakutokuwa na kuvuja au kutiririka chini au popote kwa hiyo kemikali
    • Usisafirishe kemikali za Kilimo pamoja na chakula cha binadamu au wanyama
  4. Kuhifadhi kemikali za Kilimo
    • Kama hutotumia kemikali muda huo huo, hifadhi sehemu salama na ya peke yake mbali na wanapoweza kufika watoto, watu wengine pamoja na wanyama kama paka au kuku.

Juu ya matumizi ya kemikali shambani soma pia Magonjwa ya mahindi, Makundi na faida za kemikali za Kilimo, Matumizi salama ya kemikali za Kilimo, Kuweka kemikali za Kilimo shambani, Kuchanganya kemikali za Kilimo, Kabla ya kupulizia, Wakati wa kupulizia, Baada ya kupulizia, Kutupa makopo ya Kemikali, na Kujisafisha mwenyewe na chombo cha kupulizia.