Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Kujisafisha mwenyewe na chombo cha kupulizia
Kujifanyia usafi na kusafisha dumu lako la kupulizia dawa fuata yafuatayo;
- Ukiwa bado umevaa mavazi rasmi ya kupulizia kemikali, osha dumu ulilotumia kunyunyizia kemikali na hakikisha hakuna mabaki ya kemikali yamebaki
- Mwaga maji uliyotumia kuoshea dumu kwenye ardhi tupu
- Usioshe vyombo vya kupulizia kemikali shambani karibu na vyanzo vya maji au kisimani, mtoni, bwawani au ziwani
- Jivue mavazi ya kupulizia kemikali na osha yote ukimalizia na glovu
- Osha vizuri mwili wako ukitumia maji safi na ya kutosha
- Vaa mavazi safi
- Tunza vifaa vyako vya kunyunyizia kemikali sehemu salama
- Weka kumbukumbu ya kazi yako ya kupulizia kemikali, mfano kemikali uliyotumia, ulivyochanganya, tarehe ya kupulizia, eneo/ shamba ulilopulizia na nk.
Juu ya matumizi ya kemikali shambani soma pia Magonjwa ya mahindi, Makundi na faida za kemikali za Kilimo,
Matumizi salama ya kemikali za Kilimo,
Kuweka kemikali za Kilimo shambani,
Kuchanganya kemikali za Kilimo,
Kabla ya kupulizia,
Wakati wa kupulizia,
Baada ya kupulizia,
Kutupa makopo ya Kemikali, na
Kujisafisha mwenyewe na chombo cha kupulizia.