Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Fusarium Stalk Rot

Wadudu: Fangasi: Fusarium species
Dalili:
1. Magunzi huwa na rangi ya pinki nyeupe, mabua kuvunjika na kukomaa kabla ya wakati wake
2. Kuoza huanza baad tu ya uchavushaji na huwa mkubwa mmea unapozidi kukomaa
Suluhisho/ Kutibu:
1. Panda mbegu za mahindi zenye kuweza kukabiliana na hili tatizo. Mbegu zenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na magonjwa ya majani haziathiriki sana na kuoza kwa mabua
2. Hakikisha virutubisho shambani kwako viko katika vipimo sawia, usizidishe Nitrogen na usiweke Potassium kidogo. Weka katika vipimo vinavyotakiwa
3. Kuvuna mapema pia inaweza kuwa suluhisho la kuvunjika kwa mabua kwani mazao yataweza kuvunwa kabla kuvunjika hakujatokea
4. Panda kiasi cha mahindi kinachostahili kwa ukubwa wa eneo husika, shughulikia wadudu waharibifu jinsi inavyopaswa, na hakikisha kuna mfumo mzuri wa kushughulikia maji kwenye shamba la mahindi

Soma pia: Grey Leaf Spot, Phaesosphaeria Leaf Spot, Northern Corn Leaf Blight, Northern Corn Leaf Spot, Physoderma Brown Spot, Common Rust, Southern Rust, Eyespot, Common Smut or Boil Smut, Bacterial Stalk Rot, Fusarium Stalk Rot, Gibberella Stalk Rot, Aspergillus Ear Rot, Fusarium Ear Rot, Gibberella Ear Rot, Diplodia Ear Rot, Penicillium Ear Rot, Maize Streak Virus, Maize Chlorotic Mottle virus, Sugarcane Mosaic Virus, Maize Lethal Necrosis Disease, Nitrogen Deficiency, Magnesium Deficiency, Phosphorous Deficiency, Potassium Deficiency, Pinking, Multiple Ears on Same Shank Syndrome, na Herbicide Toxicity.

Matumizi ya Kemikali Shambani

Makundi na faida za kemikali za Kilimo, Matumizi salama ya kemikali za Kilimo, Kuweka kemikali za Kilimo shambani, Kuchanganya kemikali za Kilimo, Kabla ya kupulizia, Wakati wa kupulizia, Baada ya kupulizia, Kutupa makopo ya Kemikali, na Kujisafisha mwenyewe na chombo cha kupulizia.