Mwanzo Kuandaa Shamba Mbegu & Kupanda Kutunza Shamba Kuvuna & Kuhifadhi Maswali | Majadiliano Mawasiliano & Ushauri Uza na Kununua

Kutunza Shamba

Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.

Northern Corn Leaf Spot

Wadudu: Fangasi: Bipolaris zeicola
Dalili:
1. Hutoa alama za mvirongo au zenye umbo kama yai ambazo huegemea zaidi eneo fulani la jani/ majani
2. Alama hizi huweza kuwa na rangi nyekundu-kahawia kwenye majani na maganda
3. Punje zilizo athirika huweza kuwa na rangi kama ukungu mweusi
Suluhisho/ Kutibu:
1. Panda mbegu za mahindi zenye kuweza kukabiliana na hili tatizo
2. Pulizia kemikali za kumaliza fangasi kwenye majani kama Abacus, Amistar, Bravo, Duett and Score kipindi ambapo alama zimefikia theluthi moja (1/3) ya jani kabla mhindi haujaanza kutoa maua (kuchavua)
3. Lima vizuri shamba lako na/ au endesha kilimo mzunguko kupunguza ukubwa wa tatizo

Soma pia: Grey Leaf Spot, Phaesosphaeria Leaf Spot, Northern Corn Leaf Blight, Northern Corn Leaf Spot, Physoderma Brown Spot, Common Rust, Southern Rust, Eyespot, Common Smut or Boil Smut, Bacterial Stalk Rot, Fusarium Stalk Rot, Gibberella Stalk Rot, Aspergillus Ear Rot, Fusarium Ear Rot, Gibberella Ear Rot, Diplodia Ear Rot, Penicillium Ear Rot, Maize Streak Virus, Maize Chlorotic Mottle virus, Sugarcane Mosaic Virus, Maize Lethal Necrosis Disease, Nitrogen Deficiency, Magnesium Deficiency, Phosphorous Deficiency, Potassium Deficiency, Pinking, Multiple Ears on Same Shank Syndrome, na Herbicide Toxicity.

Matumizi ya Kemikali Shambani

Makundi na faida za kemikali za Kilimo, Matumizi salama ya kemikali za Kilimo, Kuweka kemikali za Kilimo shambani, Kuchanganya kemikali za Kilimo, Kabla ya kupulizia, Wakati wa kupulizia, Baada ya kupulizia, Kutupa makopo ya Kemikali, na Kujisafisha mwenyewe na chombo cha kupulizia.