Sehemu hii tutazungumzia jinsi ya kutunza shamba la mahindi ambapo tutagusia mambo makuu manne (4) ambayo ni; nyasi na magugu shambani, mbolea, wadudu shambani, pamoja na matumizi ya kemikali shambani. Mambo haya manne yamefafanuliwa zaidi hapa chini.
Wadudu: Fangasi: Fusarium graminearum | |
Dalili: 1. Mabua mara nyingi huwa na rangi ya ndani yenye wekundu kwa tishu zilizoathirika 2. Kupasuka kwa gunzi |
|
Suluhisho/ Kutibu: 1. Panda mbegu za mahindi zenye kuweza kukabiliana na hili tatizo. Mbegu zenye uwezo mzuri wa kukabiliana na fangasi wa kwenye majani zinauwezo mzuri wa kupambana na kuoza kwa mabua 2. Hakikisha virutubisho shambani kwako viko katika vipimo sawia, usizidishe Nitrogen na usiweke Potassium kidogo. Weka katika vipimo vinavyotakiwa 3. Kuvuna mapema pia inaweza kuwa suluhisho la kuvunjika kwa mabua kwani mazao yataweza kuvunwa kabla kuvunjika hakujatokea 4. Panda kiasi cha mahindi kinachostahili kwa ukubwa wa eneo husika, shughulikia wadudu waharibifu jinsi inavyopaswa, na hakikisha kuna mfumo mzuri wa kushughulikia maji kwenye shamba la mahindi |
Soma pia: Grey Leaf Spot, Phaesosphaeria Leaf Spot, Northern Corn Leaf Blight, Northern Corn Leaf Spot, Physoderma Brown Spot, Common Rust, Southern Rust, Eyespot, Common Smut or Boil Smut, Bacterial Stalk Rot, Fusarium Stalk Rot, Gibberella Stalk Rot, Aspergillus Ear Rot, Fusarium Ear Rot, Gibberella Ear Rot, Diplodia Ear Rot, Penicillium Ear Rot, Maize Streak Virus, Maize Chlorotic Mottle virus, Sugarcane Mosaic Virus, Maize Lethal Necrosis Disease, Nitrogen Deficiency, Magnesium Deficiency, Phosphorous Deficiency, Potassium Deficiency, Pinking, Multiple Ears on Same Shank Syndrome, na Herbicide Toxicity.